Historia

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji ilianzishwa mwezi April 2016 baada ya uchaguzi mkuu na kuchukua nafasi ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya zamani.

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji ilianza kipindi cha ukoloni wakati huo ikijulikana kama Idara ya Ujenzi wa Umma ikiwa imepangiwa majukumu ya kusimamia huduma za umma, ikiwa ni pamoja na kazi, barabara, umeme, maji na makazi. Mwaka 1964, ilikuwa imegawanywa katika wizara mbili ambazo ni Wizara ya Ujenzi, Barabara na Nishati na Wizara ya Maji na Makazi.
Mwanzoni mwa mwaka 1970 Wizara ya Ujenzi, Barabara, na Nishatiikawa Wizara ya Ujenzi, Barabara na Mawasiliano wakati sehemu ya mawasiliano ya simu iliongezwa na kifungu cha nishatiikiongozwa na wizara nyingine. Katika miaka ya 1970 ilibadilishwa na kuwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ikiwa na jukumu la kusimamia maendeleo na udhibiti wa usafiri na mawasiliano.

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji inaundwa na idara sita, Ofisi kuu Pemba, taasisi huru sita na Bodi moja ya Ushauri. Idara hizo ni pamoja na Idara ya Sera, Mipango, na Utafiti, Utawala na Utumishi, Habari na Mawasiliano, barabara Uchukuzi na Leseni, ujenzi wa barabara na matengenezo Idara ya Majenzi. Taasisi huru ni Shirika la Bandari la Zanzibar, Shirika la Nyumba, Mamlaka ya Mji Mkongwe, Shirika la Meli la Zanzibar, Mamlaka ya Bahari ya Zanzibar na Mamlaka ya Ndege ya Zanzibar.Bodi ya ushauri ni Bodi ya Usafiri wa Barabara.