Sisi ni Nani?

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji inaundwa na idara sita, Ofisi kuu Pemba, taasisi huru sita na Bodi moja ya Ushauri. Idara hizo ni pamoja na Idara ya Sera, Mipango, na Utafiti, Utawala na Utumishi, Habari na Mawasiliano, barabara Uchukuzi na Leseni, ujenzi wa barabara na matengenezo na Idara ya Majenzi. Taasisi huru ni Shirika la Bandari la Zanzibar , Shirika la Meli la Zanzibar, Mamlaka ya Usafiri Baharini, Mamlaka ya Ndege ya Zanzibar, Mamlaka ya Mji Mkongwe na Shirika la Nyumba.Bodi ya ushauri ni Bodi ya Usafiri wa Barabara.

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji ilianzishwa mwezi April 2016 baada ya uchaguzi mkuu na kuchukua nafasi ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya zamani.

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji ilianza kipindi cha ukoloni wakati huo ikijulikana kama Idara ya Ujenzi wa Umma ikiwa imepangiwa majukumu ya kusimamia huduma za umma, ikiwa ni pamoja na kazi, barabara, umeme, maji na makazi. Mwaka 1964, ilikuwa imegawanywa katika wizara mbili ambazo ni Wizara ya Ujenzi, Barabara na Nishati na Wizara ya Maji na Makazi.
Mwanzoni mwa mwaka 1970 Wizara ya Ujenzi, Barabara, na Nishati ikawa Wizara ya Ujenzi, Barabara na Mawasiliano wakati sehemu ya mawasiliano ya simu iliongezwa na kifungu cha nishati ikiongozwa na wizara nyingine. Katika miaka ya 1970 ilibadilishwa na kuwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ikiwa na jukumu la kusimamia maendeleo na udhibiti wa usafiri na mawasiliano.

DIRA

Kuwa taasisi ya uma yenye kuongoza katika kujenga uchumi imara wa Zanzibar kwa kuboresha miundombinu na huduma za usafiri na mawasiliano.

DHAMIRA

Kukuza na kusimamia miundombinu na huduma za usafiri na mawasiliano zenye kukizi mahitaji ya wadau wote kulingana na viwango vya Kitaifa na Kimataifa

MAADILI MAKUU

Utiifu. Uwajibikaji. Kujitolea. Uvumbuzi. Uzalendo. Mashirikiano. Uadilifu. Uwazi.

MALENGO YA WIZARA

 • Kuridhisha wateja katika utoaji wa huduma.
 • Kuhakikisha usalama katika mfumo wa usafiri.
 • Kuhakikisha upatikanaji wa huduma za usafiri zilizobora, endelevu na zenye kuaminika.
 • Kuboresha uwezo wa taasisi katika kutoa huduma kwa ufanisi.
 • Kuhakikisha upatikanaji wa miundombinu ya usafiri na mawasiliano iyobora, salama na yenye kufanyakazi.
 • Kutoa elimu ya maambukizo ya virusi vya ukimwi kwa watumishi na wadau katika sekta ya usafiri na mawasiliano.
 • Kukuza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa taasisi zote.
 • Kuinginza masuala ya jinsia katika sekta ya usafiri na mawasiliano.

Wizara ya miundombinu na mawasiliano inajukumu la kuandaa sera, mipango na kanuni za usafiri na miundombinu ya mawasilano pamoja na huduma.

Majukumu makuu ya Wizara ni.

 • Kuaandaa na kusimamia sera, sheria, kanuni na viwango vya usafiri na TEHAMA.
 • Kupanga, kuendeleza na kudumisha miundombinu ya usafiri na mawasiliano.
 • Kuendeleza utafiti katika sekta ya usafiri na TEHAMA.
 • Kuendesha karakana kuu ya Serikali.
 • Kushajihisha mahusiano ya Serikali na taasisi binafsi katika utoaji wa huduma mbalimbali katika huduma za usafiri na mawasiliano.

Aidha, Wizara inaratibu utoaji huduma za mawasiliano ya simu, mawasiliano ya posta, elimu ya hali ya hewa na huduma za usafiri wa anga kupitia mamlaka husika chini ya Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia na Wizara ya kazi ya jamhuri ya muungano ya Tanzania.