Idara ya Utumishi na Uendeshaji.

Idara ya utumishi na uendeshaji:

Uongozi
1. Bimkubwa Abdi Nassib
Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu

Malengo makuu
1. kushughulikia kazi za kiutawala kila siku katika Wizara
2. Kujua maslahi ya wafanyakazi wa Wizara
3. Kutambua masuala yote ya uendeshaji wa Idara, ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu ya watumishi.
4. Kutambua utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka za wafanyakazi wote wa Wizara.
5. Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Wizara
6. Usimamizi wa mpango wa waelimishaji VVU na masuala ya jinsia


Aidha idara inasimamia utekelezaji wa kazi za Ofisi ya Wizara na kuhakikisha kuwa rasilimali zote muhimu zinapatikana kwa wakati na wafanyakazi kuendelea kufanya kazi katika mazingira mazuri na ya kuridhisha. Kazi kwa ajili ya ununuzi wa mashine ya ofisi (kompyuta), vifaa vya (stationeries), samani za ofisi, huduma ya malipo ya maji, umeme na mawasiliano ya simu ya ofisi (simu na mtandao). Zaidi ya hayo Idara hii hutoa huduma za usimamizi wa ofisi na kuhakikisha magari yanapata huduma na matengenezo mengine pamoja na kuyapatia mafuta .