Utiaji Saini makubaliano ya awali ujenzi wa Bandari ya Mpigaduri

Bandari ni moja ya miundombinu yenyeumuhimu mkubwa hususan kwa nchi ya kisiwa kama Zanzibar. Kwa kawaida Bandari hutumika kama mlango mkuu wa kuingizia na kutolea wageni na biadhaa muhimu kwa ajili ya mahitaji ya wananchi.

Nchi zote za visiwa duniani kama ilivyo Zanzibar, bandari huchukuliwa kama nguzo muhimu ya kiuchumi hasa katika nyanja ya uingizaji na utoaji za ndani na nje ya nchi. Zanzibar hivi sasa ina bandari tatu rasmi ambazo niWete, Mkoani na ile ya Malindi iliyopo mjini Unguja ambayo ndio Bandari Kuu na inayotegemewa zaidi katika shuhuli za usafiri za upakuaji na upakizi wa mizigo.Pamoja na kuwepo bandari hizo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina lengo la kujenga Bandari kubwa na ya kisasa ili kukidhi mahitaji ya uingizaji na utoaji wamizigo.

Hatua za awali za kuanza kwa mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Mpigaduri zimeanza baada ya tafiti mbali mbali zilizofanywa katika eneo hilo miaka kadhaa iliyopita na hivi karibuni. Bandari ya Malindi kwa hivi sasa ina uwezo wa kuchukua makontena 65,000 tu idadi ambayo haiwezi kuongezeka kutokana na ufinyu wa eneo la kuhifadhia. Baadhi ya wananchi waliohojiwa na mwandishi wa makala hii wamesema wamefurahishwa na uamuzi huo waSerikali kuamua kujenga Bandari hiyo na kuomba kuimarishwa kwa Bandari nyengine zilizopo kisiwani Pemba.

"Upanuzi wa bandari utasaidia vijana kupata ajira na hata waliomaliza skuli ambao watakaokosa ajira katika taasisi za serikaliā€, alisema Mohamed

Hassan ambaye ni mfanyabiashara anayetumia bandari ya Malindi kwa shughuli zake za kibiashara. Baadhi ya wafanyakazi wa bandari ya Malindi waliishauri Serikali kuweka vifaa vya kisasa katika bandari zote ili kurahisisha utoaji wa huduma za usafiri wa abiria na upaku mizigo.Tatizo la mrundikano wa mkontena Bandari limekua likiongezeka na limekuwa likilalamikiwa na wadau mbali mbali wanaotumia Bandari hiyo.

Mnano mwezi Februari 2014, Serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano 16 Miundombinu ilisaini mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Mpigaduri na Kampuni ya China Harbor Engineering Company (CHEC) ya China ambayo ndio itakayojenga Bandari hiyo.

Ujenzi wa Bandari ya Mpigadurihadi kukamilika kwake utagharimu dola za Marekani milioni 230.4 ambapo dola milioni 200 zinatarajiwa kuwa ni mkopo kutoka Benki ya Exim ya China na dola milioni 30.4 zitatolewa na Kampuni hiyo ya CHEC ambayo inakusudia kuingia ubia na Serikali. Azma ya Serikali pia ni kuzipanua Bandari zake nyengine zilizopo Pemba ili ziweze kufanya kazi zake kwa ufanisi ambapo zitakuwa na vifaa vya kutosha ili viweze kukidhi huduma za usafiri na kuzifanya meli mbali mbali kufunga gati na kuteremsha mizigo. Ujenzi wa Bandari ya Mpigaduri ni uamuzi wa Serikali uliokuwa ukitarajiwa kwa muda mrefu lakini ilishindikana kufanyika kutokana na ukosefu wa fedha.

Kukamilika kwa ujenzi wa bandari hiyo kutasaidia sana kupunguza msongamano uliopo katika Bandari ya Malindi, kuongeza maradufu huduma kwa meli za mizigo nakuongeza ajira na kuimarisha uchumi.