Rais aweka jiwe la msingi katika jengo la abiria Terminal II Zanzibar

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo  tarehe 9 October, 2015, aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la pili la abiria (terminal II) katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya uwekaji wa Jiwe la msingi ujenzi wa jengo jipya la Abiria Terminal II linalojengwa na kampuni kutoka China katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo,(katikati) Naibu waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (GAVU)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa nje ya jengo jipya la Abiria Terminal II linalojengwa na kampuni ya kichina katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar  na kupatiwa maelezo ya ujenzi na Msimamisi wa Mradi  kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi  Yasser De Costa, baada ya kuweka Jiwe la msingi ujenzi huo leo.