Uwekaji wa TAA na CCTV camera barabarani Zanzibar

Zitakuwa na uwezo wa kuonesha video moja kwa moja pamoja na kurekodi data ambazo zitatumika kwa ajili ya kupunguza uhalifu katika mji pamoja na kutoa taarifa kuhusu ajali za barabarani. Mfumo huu mpya utafanya kazi za maafisa wa trafiki kuwa za ufanisi na rahisi zaidi.Tofauti na sasa ambapo ushahidi kwa kosa la trafiki ni neno la afisa trafiki wa polisi tu dhidi ya dereva aliyetenda kosa, mfumo huu mpya una uwezo wa kuhifadhi ushahidi katika muundo wa dijitali ambao utatumika kwa kutoa ushahidi mahakamani.

 

Zanzibar yapiga hatua ,mafundi wakifunga Taa za barabarani pamoja na cctv camera katika eneo la mataa ya kuelekea darajani,unguja.

 

Katibu wa Kamati ya Wataalamu ya usimamizi wa Mradi wa CCTV Camera Nd. Jabir Haji Abdulla akionyesha picha mbali mbali zinazonaswa na kurikodiwa katika maeneo mbali mbali ya Mji Mkongwe.

 

 

Mounekano wa Picha tofauti zinazochukuliwa na kunaswa katika kituo cha kuongozea Camera za CCTV Malindi Mjini Zanzibar