Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe Balozi Ali Karume Aripoti kazini baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe Rais wa Zanzibar

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe Balozi Ali Karume amesema suala la umoja na ushirikiano ni muhinu katika utendaji wa kazi ili kuleta ufanisi bora  kwa kazini.
Mhe Waziri amesema haya alipokutana na uongozi wa Wizara hiyo ikiwa ni siku yake ya mwanzo kuripoti kazini tokea ateuliwe na kuapishwa na Mhe Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.Aidha alisema nidham ya kazi ni kitu kikubwa sana kazini kwani huleta heshima, mshikamano kwa wakubwa na wadogo.
Katika mazungumzo yake na wakuu wa Wizara hiyo Mhe Waziri aliwaomba wakuu hao kuwa na utaratibu mzuri wa fursa za mahitaji ya fedha na kuzijengea hija madhubuti Serikalini na sehemu zengine za mitaji na kuonesha mrejesho ulio sahihi.
 
Hata hivyo alisema upatikanaji wa fedha na matumizi yaende sambamba na lengo lililokusudiwa na sio kwenda kinyume na lengo husika.
Alifahamisha kuwa Mhe Waziri lengo la Mhe Rais kuanzisha Wizara hiyo ni kuwepo kwa uhusiano mkubwa kwa taasisi zake na taasisi zilizokuwa ktk Wizara kama hiyo ya Tanzania Bara ambazo zipo kwenye mambo ya Mungano ambapo kutarahisisha kuwa na ushirikiano mkubwa kwa kutatua kero zinazozikabili taasisi hizo.Aidha alisema Wizara hiyo kwa sasa itajikita zaidi na masuala ya ukarabati na utunzaji wa nyumba na barabara ili Zanzibar iwe na Mazingira mazuri kama yalivyo mataifa mengine.
 
Mwisho aliomba kupewa ushirikiano na kusaidiwa kazi na wakuu hao ili wawezee kufikia lengo lililokusudiwa.