Hafla fupi ya kumkabidhi ofisi Mhe waziri Mpya wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafurishaji Mhe Balozi Ali Karume

 
 
Waziri wa nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Ussi Haji Gavu amesema hakuna kitu kizuri dunia kama kuishi na watu kwa uzur kwani unaweza kujifunza mambo mengi kutoka kwa watu hao. Mhe Issa amesema hayo katika hafla fupi ya kumkabidhi ofisi Mhe waziri Mpya wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafurishaji Mhe Balozi Ali Karume katiku Ukumbi wa mikutano kisaun nje kidogo wa mji wa Zanzibar.
 
Amesema katika kipindi cha miaka 5 alichoongoza Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano alijifunza mengi kiasi ambacho hivi sana amekua zaidi ya injinia na kusahau fani yake ya sheria na diplomasia. Hata hivyo alisema mafanikio yake ameyapata kutokana na kuwa karibu na wafanyakazi wake wa ngazi zote na kukubali kupokea ushauri kila wakati. Hata hivyo aliwataka viongozi hao wapya kufuata wasia huo ili nao waweze kufaidikia na matunda hayo.
 
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi mhe Balozi amesema yupo tayari kufanya kazi mchana na usiku ili kuhakikisha wizara hiyo inafikiwa lengo