Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/2018

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mh. Balozi Ali Karume awasilisha Hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Katika hotuba yake Mh. Waziri aliomba wajumbe wa baraza tukufu la wawakilishi liidhinishe jumla ya TZS 216,820,202,000 kwa programu zake zote. Kati ya fedha hizo, jumla ya TZS 163,369,402,000 ni mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ya ujenzi wa Barabara, Viwanja vya ndege na bandari ya Mpiga Duri na jumla ya TZS 53,450,800,000 ni kutoka Serikalini, ambapo jumla TZS 9,220,800,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kazi za kawaida na jumla ya TZS 44,230,000,000 ni mchango wa Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Wizara. 

Bonyeza hapa kupata hotuba Kamili.