Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe Mustafa Aboud Jumbe akiwa Ziaran Pemba Atembelea Barabara Zilizoharibika na kutembelea maeneo yalio chini ya wizara yake
26 Sep 2018

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe Mustafa Aboud Jumbe akiwa Ziaran Pemba Atembelea Barabara Zilizoharibika na kutembelea maeneo yalio chini ya wizara yake

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe Leo Ameanza rasmi ziara ya kikazi kisiwani Pemba Kwa kutembelea sehemu mbali mbali zilizopo chini ya wizara yake.
Katika ziara hiyo ambayo alifuata na Wakurugenzi na maafisa mbali mbali kutoka wizara ya ujenzi ilikua ya mafanikio makubwa kwani aliweza kujionea mwenyewe changamoto zinazoikabili wizara yake kwa upande Wa pemba hasa kwenye sehemu za Barbara ambazo ziliathirika na mvua ambapo alisema serikali inatarajia kulitafutia ufumbuzi wa haraka hasa katka barabara za Mungu yupo na Changaweni.
Aidha katibu mkuu huyo aliweza kuitembelea barabara ya Mkanyageni - kangani ambapo alisema serikali kupitia wizara yake inajipanga kuijenga barabara hiyo ili wananchi Wa maeneo hayo waweze kuendesha shughuli zao za kijamii kwa urahisi zaidi.


Hata hivyo katibu alitembelea barabara ya Kipapo - Mgelema na Kiuyu - Ngomeni ambapo pia alisema serikali kupitia chama cha Mapinduzi inajitahidi kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa lengo lile lile la kila mzanzibar anahakikisha anapata huduma zilizobora ikiwemo miundombinu ya barabara.
Katika hatua nyengine katibu Mustafa alipata fursa ya kuitembelea barabara ya Daya - Uondwe ambapo afisa mdhamini wa wizara hiyo ndugu Ahmedi Baucha aliweza kumuonesha eneo lililoharibika kwa mvua ambapo alisema tayari wizara kupitia ofisi kuu pemba imeshaanza matayarisho ya kulifanyia matengenezo kabla ya msimu Wa mvu ujao.
Ziara hiyo itaendelea tena kesho kwa kutembelea maeneo mbalimbali kisiwani humo.

 

Last modified on Wednesday, 26 September 2018 10:00

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.