Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe Mustafa Aboud Jumbe akifanya ziara bandari ya wete kisiwani Pemba
26 Sep 2018

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe Mustafa Aboud Jumbe akifanya ziara bandari ya wete kisiwani Pemba

Katibu Mkuu Wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe amelitaka shirika la Bandari kuandaa mipango madhubuti amabayo itakayoweza kuiletea manufaa shirika hilo na serikali kwa ujumla kwa vile bandari ni sehemu moja yapo ya kuingizia kipato na kukuza uchumi Wa Zanzibar .
Katibu Mustafa ameyasema hayo alipofanya ziara bandari ya wete kisiwani Pemba ambapo alijionea eneo ambalo linalo tarajiwa kujengwa bandari na muekezaji mzalendo mara tu mipango itakapo kamilika.
Hata hivyo amesema endepo bandari hiyo itajengwa itaweza kuwafanyiwa wepesi Wa usafiri wananchi Wa mkoa Wa kaskazini Pemba kwa vile wameikosa huduma hiyo kwa muda mrefu sasa kutokana na miundombinu duni iliyopo hivi sasa.
Aidha katika mfululizo wa ziara zake kisiwani hapa katibu mkuu huyo aliweza kutembelea barabara ya wete - gando ambapo alipata maelezo sehemu ya Mangwena kutoka kwa injinia mkaazi khamis Masoud juu ya hitlafu ilijitokeza kwa kuporomoka kutokana na mvua zilizopita.
Kutoka na hali hiyo katibu mkuu amesema serikali inachukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha njia hiyo inajengwa ili ipitike kama zaman kwa vile ni kiungo kikubwa kwa wananchi waishio maeneo ya gando.
Aidha katibu mkuu huyo aliweza kupitika eneo la kizimban Ambapo alikagua Ujenzi wa kalvat unaendelea hivi sasa na kuridhishwa na Ujenzi huo.
Katika ziara hiyo pia alipita kwenye mnara Wa kigomasha ambapo alisifu jitihada zilichukuliwa na shirika la bandari la kupaimarisha kwa usalama wa vyombo vya baharini.
Mapema asubuh katibu mkuu huyo alihudhuria site visit barabara ya Ole - Kengeja na kufanya kikao cha steering commitee kwa lengo la kupitia na kuimarisha mradi huo ili uweze kumalizika kwa wakati.

 

 

 

 

 

 

 

Last modified on Wednesday, 26 September 2018 11:35

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.