Ziara ya kutembelea mradi wa OLE-KENGEJA na kuangalia hatua zinazoendelea za ujenzi wa Barabara hiyo tarehe 26/11/2018.
Makutano ya Barabara ya Mfikiwa Pemba

Ujenzi wa daraja maeneo ya Pujini katika mradi wa Barabara ya OLE -KENGEJA.

Picha ya pamoja kati afisa ufuatiliaji kutoka OFID Bwana Sharaighm Shams na watendaji wa Mradi wa OLE-KENGEJA.
TAARIFA KAMILI
Afisa ufuatiliaji kutoka mfuko Wa Fedha za maendeleo ya kimataifa OFID bwana Sharaighm Shams ameeleza kufurahishwa kwakwe kwa hatua nzuri iliyofikiwa kwenye Ujenzi Wa barabara ya Ole -Kengeja inayoendelea kwa kasi hivi sasa.
Afisa huyo ameyaleza hayo mara tu baaada ya kutembelea mradi huo ambapo alikutana na watendaji Wa mradi huo pamoja na Mshauri msimamizi Kapsel, aidha baada ya ziara hio alifanikiwa kukaa na watendaji na kujadiliana kuhusiana na mradi huo, na kuweza kuangalia namna gani wanaweza kutatua changamoto zinazoikabili mradi huo.Hata hivyo amesema anafahamu kuwa mradi huo kuwa Wa miaka mingi lakini ameeleza kuwa iman yake mradi huo kwa hivi sasa utandelea vyema ili uweze kumaliza na ibaki historia tu.
Sambamba na hayo afisa huyo amesisitiza kuwa wizara ijitahidi kutekeleza mahitaji muhimu ya wananchi ambao wamepitiwa na Mradi huo ili kuhakikisha wananchi hao wanafaidika na mradi huo, pamoja na kuengeza uwezo kwa wafanyakazi Wa wizara pamoja na vibarua.
Kwa upande wake meneja mradi Amini khalid amesema amefarajika sana kupata ugeni kwa kuja kuangalia Ana kwa Ana mradi huo ili kujiona hatua zilizofikia. Aidha alisema mara nyingi wamekuwa wakiwasiliana tu kwa njia za mitandao lkn ujio huo umeweza kuleta mwamko na uhalisia zaidi Wa kazi zao. Hata hivyo amesema muda mfupi Wa ugeni huo wameza kujifunza mambo mengi ambayo yanayofurahiwa na mfadhili ikiwa pamoja na kukua kwa uchumi Wa jamii.