Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Dr Sira Ubwa Mamboya amezindua rasmi mfumo mpya wa kutolea huduma za Kibenki
02 Jan 2019

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Dr Sira Ubwa Mamboya amezindua rasmi mfumo mpya wa kutolea huduma za Kibenki

 

 

UZINDUZI WA MFUMO MKUU WA KUTOLEA HUDUMA ZA KIBENKI (BENKI YA WATU WA ZANZIBAR PBZ), KATIKA SHAMRA SHAMRA ZA MIAKA 55 YA MAPINDUZI.

 

Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Dr Sira Ubwa Mamboya amezindua rasmi mfumo mpya wa kutolea huduma za Kibenki siku ya tarehe 2/1/2019 ikiwa ni katika Shamra Shamra za maadhimisho ya miaka 55 ya  Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Mfumo ambao ni maboresho wa mfumo ambao uliokua ukitumika hapo kabla na utasaidia kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto za foleni kubwa ya watu wakisubiri huduma hususan katika siku za mwisho wa mwezi, kuzidiwa kwa utendaji wa Mashine za kutolea pesa (ATM) na utasaidia kupatikana kwa huduma nyengine muhimu kwa wateja wake pamoja na huduma ya kadi za Kimataifa kama vile za Visa na Mastercard ,Mfumo huu utawezesha kuweka, kutoa na kuhaulisha pesa kwa kutumia “internet” – hakuna haja ya wateja wenye huduma hiyo kwenda katika matawi ya PBZ.

 

Wataweza kufanya yote hayo wakiwa nyumbani au katika ofisi zao. Mtandao utawezesha malipo ya huduma mbalimbali kama kulipia umeme, maji, ada za Serikali kupitia Huduma za Simu za Mkononi. Kwa sasa huduma za Benki zitapatikana kwa saa 24 siku zote, huduma za ATM zitakuwa na ufanisi zaidi na huduma nyingi ambazo hazitohitaji mteja kwenda tawi la Benki. Mfumo huu umebuniwa na Kampuni ya ICS Financial Sytem kutoka Jordan.

 

Mheshimiwa Mgeni Rasmi Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Dr Sira Ubwa Mamboya akitoa hotuba katika uzinduzi wa mfumo wa utoaji wa huduma za Kibenki

 

Mheshimiwa Mgeni Rasmi Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Dr Sira Ubwa Mamboya akizindua rasmin mfumo mpya wa kutolea huduma za Benki

Mheshimiwa Mgeni Rasmi Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Dr Sira Ubwa Mamboya akiwa katika picha ya pamoja ya Viongozi na  Wafanyakazi wa PBZ

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.