Majumuisho ya Kufunga Mradi wa Mageuzi ya Taasisi za Wizara
06 Feb 2019

Majumuisho ya Kufunga Mradi wa Mageuzi ya Taasisi za Wizara

Waziri Wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dkt Sira Ubwa Mamboya akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wakuu Wa Tasisi za Wizara yake na kampuni ya ICT baada ya kufungua rasmi kikao cha siku moja cha majuisho ya mageuzi ya Wizara.

Waziri Wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dkt Sira Ubwa Mamboya amesema utekelezaji Wa mradi Wa mageuzi ya Wizara yake unatarajiwa kuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kupunguza urasimu na kuongeza ufaninisi katika utoaji wa huduma za usafiri hapa Zanzibar. 

Dkt Sira ameyasema hayo Leo alipokua akifungua mkutano Wa siku moja Wa majumuisho ya mradi Wa mageuzi ya Taasisi za wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji huko katika ukumbi Wa Zanzibar Beach Reasort.
Aidha alisema mpango huo pia utasaidia kuwepo kwa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika utoaji Wa huduma za miundombinu ya usafiri kama inavyosisitizwa na sera za ushirikiano baina ya sekta binafsi na sekta ya umma.
Hata hivyo alisema kuwepo na ufanisi katika udhibiti na usimamizi wa sekta ya usafiri,elimu kwa madereva na watumiaji wa barabara na kupelekea kuongezeka Kwa kiwango cha usalama na kupungua kwa ajali za barabarani.
Sambamba na hayo Mhe Waziri kwa niaba ya Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi aliishukuru kampuni ya ICT kutoka India kupitia kiongozi Wa kazi ya mageuzi Dr Adoo Abeid kwa kazi nzur na kubwa waliyoifanya na kuweza kuacha muongozo wa kuufuata katika utekelezaji Wa mradi huu Wa mageuzi.Aidha alisema pamoja na kumalizika kwa mradi huu wizara itaendelea na juhudi za kukamilisha mageuzi haya kama ilivyopendekezwa na wataalam hao kwa vile kazi kubwa imeshafanyika.
 
Mkutano huo Wa siku moja ambao lengo lake kubwa ni kujitathmini juu ya utekelezaji Wa mradi Wa mageuzi ambao wizara umeutekeleza takriban kwa kipindi cha miaka minne Kwa kuzingatiwa mpango mkuu Wa usafiri Zanzibar ambapo uliidhinishwa rasmi na Serikali mnamo mwaka 2008 /2009.

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.