Uzinduzi wa Barabara ya Mkanyageni Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba
21 Feb 2019

Uzinduzi wa Barabara ya Mkanyageni Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa Kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Barabara ya Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba leo.kushoto Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Mhe. Sira Ubwa Mwamboya. 

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Zanzibar Ndg. Mustafa Aboud Jumbe, akisoma taarifa ya kiufundi ya ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami kutoka Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba, baada ya kufunguliwa barabara hiyo leo.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe. Dr. Sira Ubwa Mamboya, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Barabara ya kiwango cha lami katika Kijiji cha Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba, kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kuhutubia katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Barabara. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba,wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Barabara iliojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba.

 

 

 

 

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.