Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa SMZ Mhe. Dkt Sira Ubwa Mamboya atembelea TTCL
09 Apr 2019

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa SMZ Mhe. Dkt Sira Ubwa Mamboya atembelea TTCL

 

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (kushoto) akizungumza mara baada ya ziara yake kutembelea  Miundombinu na Mitambo ya Mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba akiwa na mgeni wake. 

 

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dkt Sira Ubwa Mamboya amelitaka Shirika la  Simu la Tanzania( TTCL) kuhakikisha linatoa huduma zilizobora na rahisi kwa manufaa ya watanzania ili waweze kuutumia mtandao huo bila ya usumbufu.

Dkt Sira ameyasema hayo Leo huko makao makuu ya Shirika hilo jijini dar es Salam alipofanya ziada maalum ya kikazi kwa lengo la kutaka kujionea Mitambo inayounganisha Mkonga Wa Taifa kutoka Dar es salam hadi Zanzibar.

Aidha alisema lengo la ziara hiyo ni kujifunza namna mitambo ya Mkonga huo wa Taifa unavyofanya kazi zake kwa pamoja katika kuwaletea urahisi wananchi na Serikali kwa jumla.

Hata hivyo alisema Mkonga Wa taifa umekua ukirahisisha mambo mengi sana hasa katika Taasisi za Serikali ambapo alisema Serikali bila ya Mkonga haiwezi kufanya kazi zake kwa ufahanisi.

Dkt Sira alifahamisha kuwa Mkonga Wa taifa pia umeufanya ulimwengu wa Mawasiliano kuwa  rahisi zaidi kwani umeweza kuunganisha wananchi kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania. Aidha alisema kwa vile shirika hili la simu ni shirika ambalo lipo katika sehemu ya muungano atahakikisha anachukua changamoto zinazokabili shirika hilo na kuzipeleka ngazi za juu zaid ili ziweze kutatuliwa kwa haraka.Aidha dkt Sira alitoa angalizo kwa mkurugenzi mkuu Wa shirika hilo ahakikisha mawasiliano yanapatikana vyema na hata ikitokea hitlafu yoyote sababu isiwe ya TTCL kwani alisema TTCL ndio tegemeo la wanyonge.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Wa Shirika Hilo Ndugu Waziri Kibamba amesema  kama  kiongozi mkuu Wa shirika hilo hatoruhusu shirika hilo kufanya kazi kwa uzembe na mzaha katika kusimamia Mawasiliano ya nchi.Hata hivyo alisema licha ya changamoto zilizopo katika shirika hilo,Shirika lipo Imara na tayari wametoa gawio la faida kwa serikali zaid ya billion 1.2 kwa mwaka Jana na mwaka huu wanategemea kutoka gawio jengine bilion 2 ili ziweze kusaidia maendeleo mbali ya nchi. 

Katika ziara hiyo Dkt sira ambae alifuatana na mkurugenzi Wa Mawasiliano Zanzibar Dkt Mzee Sleiman Ndewa pamoja na Maafisa kutoka wizara ya Ujenzi Znz alipata fursa ya kutembelea kituo cha  usimamizi Wa mtandao kilichopo posta pamoja na kituo cha kuhifadhi Wa mitambo ya Mkonga TANESCO Ubungo jijini dar es Salam.

 

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.