Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kupitia Wizara yake ya ujenzi mawasiliano na usafishaji imepokea vifaa vya ujenzi wa barabara
19 Jun 2019

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya ujenzi mawasiliano na usafishaji imepokea vifaa vya ujenzi wa barabara

 

 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kupitia Wizara yake ya ujunzi mawasiliano na usafishaji imepokea vifaa vya ujenzi wa barabara kwa ajili ya ujenzi wa barabara mbalimbali za Unguja na Pemba ambavyo vimegharimu zaidi ya shilingi bilioni 14.

Akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi Idara ya Utunzaji na Utengenezaji Barabara UUB Ali Twahir Fatawi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kununua vifaa hivyo vya ujenzi wa barabara ili kupunguza gharama za ujenzi kutoka kwa wakandarasi wa kampuni za kigeni.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe ametembelea mtambo wa kuzalisha lami unaojengwa eneo la Kibele mkoa wa Kusini Unguja na kuelezea jinsi utakavyosaidia Serikali kupunguza gharama za Ujenzi wa miundombinu ya Barabara.

Vifaa vilivyo wasili ni pamoja na vijiko 3, Greda 4, Excaveter 4, Shindilio 3 Doza 1 pamoja na mtambo huo wa lami ambavyo vinatarajiwa kurahisisha utendaji kazi kwenye miradi ya Barabara na kuweza kukamilika kwa wakati uliopangwa.

 

 

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.