Mhe. Waziri akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi wa mfuko wa mawasiliano kwa wote pamoja na baadh y wajumbe wakati akiwasili katika ofisi za mfuko huo
Mnara wa Mawasiliano uliopo Makanda, wilaya ya Bahi Dodoma
Kikao cha pamoja baina ya mhe. Waziri, wajumbe wa bodi pamoja na watendaji wa mfuko wa mawasiliano kwa wote
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar amefanya ziara Dodoma kuangalia Miradi mbali mbali inayotekelezwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Katika ziara hiyo Mhe. Waziri alikutana na Waziri, Naibu Waziri pamoja na Watendaji wengine wa Wizara.Aidha Mhe. Waziri alipata nafasi ya kutembelea mnara wa kurusha mawasiliano wa Makanda ambao upo Wilaya ya Bahi katika Mkoa wa Dodoma kituo ambacho kimejengwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF ili kusaidia upatikanaji wa mawasiliano katika maeneo hayo.