Waziri wa Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Dr Sira Ubwa Mamboya  ametembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
13 Aug 2019

Waziri wa Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Dr Sira Ubwa Mamboya ametembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Mheshimiwa Waziri akiwa katika ofisi za TCRA kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA Bibi Connie Francis

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Dr Sira Ubwa Mamboya  ametembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa ni muendelezo wa ziara yake aliyoanzia dodoma . Akiwa katika Ofisi hizo amepata fursa ya kujionea na kufahamu shughuli mbali mbali zinazotekelezwa na Mamlaka hiyo.

Aidha alitembelea makumbusho yaliyomo ndani ya Mamlaka hiyo na kuona jinsi hatua zilizopitiwa katika njia mbalimbali ambazo zilikua zikitumika hapo awali katika mawasiliano hadi kufikia hivi sasa tukiwa katika mifumo ya kisasa.

Mhe. Waziri alitembelea gari maalum liliopo ofisini hapo lenye mitambo ambayo yanawezesha kufatilia matumizi ya masafa ya mawasiliano

Katika hatua nyengine Mheshimiwa Waziri ametembelea Shirika la Posta la Tanzania( TPC)  na kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na Shirika hilo pamoja na kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa Shirika hilo.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Dkt Sira Ubwa Mamboya (wa pili kushoto) akisikiliza maelekezo na kuangalia gari lenye mtambo maalum (halipo pichani) wa kufuatilia matumizi ya masafa kutoka kwa mtaalamu wa TCRA wakati wa ziara yake kwenye Taasisi hiyo.

Gari maalum lenye mtambo wa kufuatilia matumzi ya masafa ya mawasiliano.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji. Dkt Sira Ubwa Mamboya (katikati) akiongea na Bodi na Menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Dkt Haruni Kondo.

Mheshimiwa Waziri akiwa katika kikao cha pamoja na watendaji wakuu wa Shirika la Posta Tanzania.

Mheshimiwa Waziri akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Shirika la Posta, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Dkt Kondo, kulia ni Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Atashasta Nditiye na anaefuata ni Postmaster General Ndugu Hassan Mwang’ombe.

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.