Ziara ya kamati ya Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi
21 Aug 2019

Ziara ya kamati ya Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi

Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano mhe Hamza Hassan Juma ameitaka kampuni ya simu ya mkononi Zantel kutoa huduma zilibora zaidi kwa wananchi ili waweze kujenga iman na kampuni hiyo.

Mhe Hamza ameyasema hayo leo alipokutana na uongozi wa juu wa kampuni hiyo ya zantel kwa lengo la kutaka kujua changamoto mbali mbali zinazokabili kampuni hiyo pamoja mafanikio yanapatikana.

 Aidha mwenyeketi huyo ameitaka kampuni hiyo kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo kwa mtandao wa zantel kwa vile kumekua na kesi nyingi zinazotokana na mtandao wa zantel.

hata hivyo mhe Hamza alitaka kujua suala la Minara hali ikoje kwa vile maeneo mingi katika visiwa vya Unguja na Pemba kumekua na ukosefu mkubwa wa huduma hiyo jambo ambalo linawasababishia usumbufu wa Mawasiliano kwa watumiaji wa mtandao huo.

Mwenyeketi huyo alitaka kujua suala la ajira likoje maana kwenye maeneo mengi wanayopita wameona vijana walipo katika sehemu hizo ni kutoka Tanzania Bara wakati wapo vijana wengi sana hapa Zanzibar  wana sifa.

sambamba na hayo mhe hamza ameijulisha Kampuni hiyo kuwa hivi sasa serikali imeanzisha wakala  wa mkongo na matumaini yake kwamba hakutakua na maingiliano kati yao. 

kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha mawasilino na Technolojia bwana John Sicilima,   ameipongeza sana serikali kwa kuanzisha wakala wa mkongo wa taifa  na wanaiomba serikali kuiwezesha wakala hiyo ili iweze kufanya kazi zake kama ilivyokusudiwa na kuahidi kutoa mashirikiano ya hali ya juu.

akijibu kuhusu Minara amesema tayar kampuni yao  imejipanga kujenga  Minara katika maeneo ambayo yana shida ya mawasiliano kwa maeneo korofi kwa Unguja na Pemba.

aidha amesema kampuni yao pia imejipanga kwenda na wakati na wateja wao kwa kuhakikisha wanaboresha huduma za 2G,3G na 4G ili waweze kutumia huduma ya internet bila ya vikwazo vyovyote.

sambamba na hayo bwana Sicilima,amesema kuhusu ajira kwenye kampuni yao imekuwa na makubaliano na vyuo vikuu ya hapa Zanzibar kikiwemo chuo Kikuu cha Zanzibar na chuo cha Karume kwa kuchukua wanafunzi 85 kila baada ya miezi 6 lengo hasa ni kutoa ajira kwa vijana wa kinzanzibar .

 

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.