Taarifa Ya Utekelezaji wa Bajeti kwa robo ya nne ( APRIL – JUNE 2019) kwa kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi
31 Aug 2019

Taarifa Ya Utekelezaji wa Bajeti kwa robo ya nne ( APRIL – JUNE 2019) kwa kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi

 

 

Kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi

Watendaji wakuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wakati wa uwasilishaji wa ripoti kwa Kamati ya Baraza la Wawakilishi

 

Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi imeridhishwa na taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa robo ya nne APRIL-JUNE 2019 ya Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar. 

Akisoma taarifa hiyo Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dr Sira Ubwa Mamboya amesema,Wizara katika kipindi hicho imeweza kukamilisha miradi mbali mbali ikiwa pamoja na kikamilika kwa kazi ya uwekaji wataa  za kuongozea magari katika maeneo matano ambayo ni Mlandege (Muzammil Center), Mtoni na Biziredi kwa upande wa Unguja, Mtemani Wete na PBZ Chake kwa upande wa Pemba.

Pia kwa upande wa huduma za meli Wizara imekamilisha ujenzi wa meli ya Mafuta ya MT Ukombozi II iliyojengwa na Kampuni ya Damien Shipyard ya Uholanzi

Aidha Wizara imefanikiwa kuanzisha wakala wa kusimamia Mkonga wa taifa wa mawasiliano ,pia kwa upande wa mamlaka ya viwanja vya ndege mradi wa ufungaji wa mashine za upekuzi ambapo mashine nne kati ya tano zimeshafungwa , aidha ujenzi wa miundombinu katika eneo la kuweka mashine moja iliyobakia inaendelea na mara tu baada ya kukamilika ujenzi huo mashine hiyo itafungwa.

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.