Ziara ya Mhe Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji katika Barabara ya BAHANASA – MTAMBWE NA OLE-KENGEJA. (PEMBA)
01 Sep 2019

Ziara ya Mhe Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji katika Barabara ya BAHANASA – MTAMBWE NA OLE-KENGEJA. (PEMBA)

 

Site Engineer  Ndugu Mohamed Mzee Mohamed akitoa  maelezo kwa mh waziri juu ya ujenzi wa barabara ya ole kengeja

kazi za ujenzi wa barabara ya ole kengeja zikiendelea ambapo zimebaki kilomita saba kumaliziwa kusafishwa

 

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji alifanya ziara katika Barabara ya Bahanasa – Mtambwe mnamo tarehe 1/09/2019 kuangalia eneo la Kisalani ambalo limeharibika kutokana na mmong’onyoko wa udongo hadi kupelekea nusu ya sehemu ya barabara kutoweza kupitika, eneo hilo tayari limeshafanyiwa upembuzi yakinifu na Kampuni ya Dar- Alhandasi ya Lebanon na pia Wizara tayari imefanya makisio ya kuanza kulitengeneza eneo hilo.

Aidha Mheshimiwa Waziri alitembelea Barabara ya Matuule- Kele- Bagamoyo ambayo wananchi wa Chambani kupitia Muwakilishi wao wameomba itumike kama njia ya muda wakati wakisubiria kutengenea kwa eneo la Kisalani.

Pia Mhe. Waziri alitembelea Barabara ya Ole-Kengeja kuangalia maendeleo ya mradi huo ,hata hivyo  amefurahishwa na kasi ya ujenzi huu ambapo kazi zinazoendelea kwa sasa ni uwekaji wa kifusi daraja la kwanza pili na la tatu kutoka Chambani hadi Ukutini (5km) kwenye maeneo yote yasiyokuwa na vikwazo, Ujenzi wa madaraja mawili (2), Daraja la Chambani (Shangini) na Daraja la Ukutini (kwa Kichwa), Usafishaji na utayarishaji wa tuta la barabara kutoka Ukutitini hadi Kendwa (7km) nao unaendelea. Sambamba na kazi hizo, matayarisho ya uwekaji wa lami kwa eneo ambalo tayari limewekwa lami nyepesi (2.7km) yanaendelea. Kwa sasa utekelezaji wa mradi huu umefikia 61%.

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.