Hafla ya ufungaji warsha  ya siku mbili kwa wadau wa barabara kutoka nchi za ukanda wa Africa Mashariki
19 Sep 2019

Hafla ya ufungaji warsha ya siku mbili kwa wadau wa barabara kutoka nchi za ukanda wa Africa Mashariki

 

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Barabara akifuatiwa na Mkurugenzi Fedha wa Mfuko huo.

Mgeni rasmi Mhe. Mohammed Ahmada Salum akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya wadau wa Barabara pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa Barabara – Zanzibar.

Mheshimiwa Naibu Waziri katika picha ya pamoja na watendaji wa Mfuko wa Barabara.

 

Naibu waziri wa ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji mhe Mohammed Ahmada amesema iwapo barabara zitatunzwa na kupewa fedha kutoka taasisi husika kwa ajili ya kuziboresha barabara hizo kuna uwezekano mkubwa wa kufikia malengo ya dira ya 2020,Mkuza lll ,pamoja na ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Naibu waziri huyo ameyasema hayo jana alipofunga rasmi warsha ya siku 2 kwa wadau wa barabara kutoka nchi za ukanda wa Africa Mashariki huko katika  hotel ya Madinatul Bahari Mbweni mjini Zanzibar.
Aidha amesema nchi hizi zimekua na utaratibu  wa kukutana na kukaa pamoja  ili kuangalia mifumo inayofanana kwa ujenzi wa barabara na utunzaji ili ziweze kuwa na mfumo sawa.
 
Hata hivyo alisema kwa hapa Zanzibar mfuko wa barabara unajukumu la kutoa fedha kwa wizara ya ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji na wizara ya TAMISEMI ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa ajili ya kuzifanyia matengenezo barabara kubwa na barabara za ndani. 
kwa upande wake mshiriki wa warasha hiyo  mhandisi Fares Ngereja kutoka Halmashauri ya Mkoa wa Kigoma amesema warsha hiyo ya siku mbili  imewawezesha kujua namna bora ya ujenzi wa barabara na madaraja kwa urahisi zaid jambo ambalo litawafanya waweze kuokoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi huo. 
 
Nae Injinia Khamis Masoud mshiriki wa mafunzo hayo kutoka kisiwan Pemba amesema alichojifunza katika warsha hiyo wameshauriwa kutumia ujenzi wa labour base ambapo wanajivunia kwa upande wa zanzibar tayari wameshaanza kutumia mfumo huo tokea zaman.
Aidha alisema pia waliweza kufundishwa namna ya kujenga madaraja kwa kutumia mawe na kuacha na nondo ambapo alisema mpango huo ni mzuri na ingeweza kupunguza matumizi ya fedha nyingi lakini kwa uhalisia wa visiwa vya Unguja na pemba mpango huo hauwezekani kwa  kuwa hakuna mawe mazito yatakayoendana na Technolojia hiyo 

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.