Uwekaji saini mkataba na kampuni ya mawasiliano ya zantel na wakala wa Mkonga Zanzibar
10 Sep 2020

Uwekaji saini mkataba na kampuni ya mawasiliano ya zantel na wakala wa Mkonga Zanzibar

Naibu Waziri  Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe. Mohammed Ahmada akishuhudia makabidhiano ya mkataba wa kuunganishwa kwenye mkongo wa Taifa kati ya Pemba na Tanga kuboresha mawasiliano kisiwa cha Pemba, wakitia Saini Mkuu wa Zantel-Zanzibar,Ndg. Mohammed Mussa Baucha na (Kulia) Mkurugenzi wa Wakala wa Miundombinu ya Mawasiliano (Tehama), Mhandisi Shukuru Suleiman (kushoto).Hatua hiyo itasaidia kuboresha huduma za mawasiliano visiwani humo.

 

UWEKAJI SAIN

Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji mhe Muhammed amesema sekta ya TEHAMA ni sekta muhimu sana ambayo kwa kiasi kikubwa inawezesha taifa kufikia katika uchumi wa kati napia imo katika mipango na mikakati ya vision 2020.

Naibu waziri huyo ameyasema hayo leo baada ya utiaji saini mkataba na kampuni ya mawasiliano ya zantel na wakala wa Mkonga Zanzibar juu ya upitishaji mkonga kutoka Tanga hadi Pemba huko katika ukumbi wa mikutano kisauni nje kidogo wa mji wa znz.

Aidha alisema katika mkuza III wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka sekta ya mawasiliano katika daraja la juu ili kuhakikisha sekta iyo inafanya vizur kwa vile Serikali inategemea sana kukuza pato la taifa kupitia sekta hii.

Hata hivyo alisema iman yake kubwa mfumo huo ulioanzishwa utakwenda kama ilivyokusudiwa ili kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa hii ya wasiliano wakati wowote anaouhitaji bila ya kupata changamoto zozote.

Naibu waziri huyo alifahamisha kuwa miundombinu ya Tehama imekua chachu ya maendeleo kwa vile hivi sasa mkonga umeanza kutumika kwa njia ya E HEALTH njia ambayo imeanza kutumika katika hospt ya makunduchi na mnazimoja kwa kuwasiliano namna na kutibu mgonjwa bila ya kukutana na matibabu yanafanyika bila ya shaka yoyote.

Aidha aliitaka kampuni ya zantel kuzidisha mashirikiano kwa Serikali ya Mapinduzi ya Znz kupitia wakala wake wa mkonga kwa kusaidia kutoa huduma iliyobora kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe amesema lengo kuu la Seriakali kuanzisha Wakala wa Mkonga hapa Zanzibar ni kujenga mahusiano mazuri kwa wadau wote wa mawasiliano na hadi hivi sasa wakala huo umekua ukienda vizuri katika kutekeleza majukumu yao.

Nae Mkurugenzi wa Wakala wa Mkonga wa Serikali Zanzbar Shukuru Awadh Sleiman a meitaka kampuni ya zantel baada ya mkataba huo kusainiwa iwapunguzie gharama za internet ili kila mwananchi aweze kuhimili kutumia internet kwa urahisi Zaidi.

Kwa upande wake muakilishi kutoka zantel ndugu Ahmed Baucha amesema kuunganishwa kwa mkonga wa taifa kutoka Tanga hadi Pemba kutawezesha kupatikana kwa huduma ya zantei bila ya shida ukilinganisha na hapo awali ambapo kilikua kilio cha wananchi wengi walioko kisiwan PEMBA.

Aidha alisema lengo kuu la kampuni yao ni kudumisha kutoa huduma zilizo bora na sio bora huduma ili kuhakikisha uchumi wa nchi unakua kwa kuweza kupata wateja wengi na kuweza kulipa kodi kwa serikali kwa vile kodi ni chanzo kikubwa cha mapato ya nchi.

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.