Ziara ya Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi shirika la Bandari Zanzibar
15 Mar 2021

Ziara ya Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi shirika la Bandari Zanzibar

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mh Rahma Kassim Ali akikagua kitabu Cha malipo Cha shirika la bandari maeneo ya funguni

 

Waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Mh Rahma Kassim Ali akipokea changamoto kwa mawakala wanaoleta mkaa na magogo bandari ya funguni mjini unguja 

 

Wizara ya Uenzi  Mawasiliano na uchukuzi imeutaka uongozi wa shirika la bandari Zanzibar kuhakikisha malipo yote yanayofanywa kwenye bandari ya majahazi  eneo la Funguni Unguja  yanalipwa  kwa njia ya benki ili kuepusha uvujaji wa mapato kwenye  bandari hiyo.

Waziri wa ujenzi  Mawasiliano na Uchukuzi  Rahma Kassim Ali ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea bandarini hapo na  kutorishwa na  mfumo unaotumika katika malipo ya huduma mbalimbali katika eneo hilo.

Akizungumza  baada ya kutembelea maeneo hayo Waziri wa Ujenzi mawasiliano na uchukuzi Mh. Rahma Kassim Ali amesema serikali imekuwa ikisisitiza ukusanyaji mapato ili kuinua uchumi hivyo ni wajibu wa watendaji  kusimamia vyema mapto ya serikali kwenye maeneo yote ya bandari.

Nao wananchi wanaofanya shughuli ya ushushaji mizigo katika bandari hiyo wameomba uongozi wa Wizara hiyo kutataua changamoto zinazojitokeza katika bandari hiyo.

Katika ziara hiyo  Waziri wa Ujenzi Mawasilaino na Uchukuzi alitembela pia bandari ya majahazi Malindi pamoja na Tawi la Benki ya watu wa Zanzibar Bandarini kujionea jinsi huduma za malipo zinavyofanyika.

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.