Ziara ya Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi katika jengo la Terminal III Uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar
16 Mar 2021

Ziara ya Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi katika jengo la Terminal III Uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar

Picha ya pamoja Kati ya wasimamizi na wajenzi wa jengo la abiria Terminal III na uongozi wa Wizara.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mh Rahma Kassim Ali akipokea maelezo ya kitaalam kwa msimamizi na mkaguzi wa jengo hilo Gordon Chigudul

 

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe Rahma Kassim Ali amesema kumalizika kwa jengo jipya la abiria la terminal iii (BCEG) kutaondosha msongamano uliopo na kuimarisha utoaji huduma katika eneo hilo.

Akizungumza wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo Mh Rahma amemsisitiza mkandarasi wa ujenzi huo kuhakikisha wanamaliza kazi zilizobaki kama ilivyo katika makubaliano ya mkataba wao.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo Amour Hamil Bakari amesema kabla ya kukabidhiwa kwa jengo hilo watawapatia mafunzo wafanyakazi ambao wanategemea kufanya kazi hapo ili kujua mifumo iliyopo katika jengo hilo.

Kwa upande wake msimamizi wa jengo hilo kutoka kampuni ya ADPI ya ufaransa  amesema hadi sasa kazi yote iliyofanyika ni asilimia 96 na asilumia 4 ni kazi ndogo ndogo za ndani na nje ya jengo pamoja na kurekebisha mifumo ya AC na mikongo.

 

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.