UTIAJI SAINI WA HATI YA MAKUBALIANO YA  AWALI KATI YA WIZARA YA UJENZI MAWASILIANO NA UCHUKUZI ZANZIBAR NA KAMPUNI YA NET GROUP YA ESTONIA
20 Mar 2021

UTIAJI SAINI WA HATI YA MAKUBALIANO YA AWALI KATI YA WIZARA YA UJENZI MAWASILIANO NA UCHUKUZI ZANZIBAR NA KAMPUNI YA NET GROUP YA ESTONIA

Mkurugenzi Idara ya Mawasiliano Mzee Suleiman Mndewa kulia na kushoto ni meneja wa kampuni ya Net Abeid Zagar wakitia saini mkataba huo

Picha ya pamoja baina ya watendaji wa Idara ya Mawasiliano na watendaji wa kampuni ya Net Group.

Picha ya kikao Cha pamoja Cha utiaji  saini Kati ya Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi kupitia Idara ya Mawasiliano na kampuni ya Net Group yenye makao makuu yake nchini Estonia

 

Wizara ya ujenzi mawasiliano na uchukuzi Zanzibar kupitia Idara ya Mawasiliano imetiliana saini mkataba wa awali wa mashirikiano wa ujengaji Smart Hub na kampuni ya Net group yenye makao makuu yake nchini Estonia.

Akizungumza baada ya utiaji saini huo Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano dkt Mzee Suleiman Mndewa amesema mfumo huo wa teknologia wa smart hub utarahisisha utendaji kazi katika taasisi mbali mbali nchini hasa bandari na airport.

Mshauri elekezi wa kampuni ya net group Bakari Mohamed amesema kampuni hiyo itatoa mashirikiano kwa Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar kwa kuwashirikisha wataalam wa Wizara ya Ujenzi ili wawapatie ujuzi na kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Nae meneja wa kampuni hiyo bwana Abeid Zagar amesema lengo hasa la mkataba huo ni kukuza kipaji cha software kimaendeleo na vipaji vya vijana ambao watapatiwa mafunzo mfumo huo.

 

 

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.