Uzinduzi wa kurejesha huduma katika Kiwanja cha Ndege Kigunda
08 Apr 2021

Uzinduzi wa kurejesha huduma katika Kiwanja cha Ndege Kigunda

 

 

Daktari wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege akiwapima joto wageni wanaotaka kusafiri katika Uwanja wa Kigunda Mkoa wa Kaskazini Unguja 

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inampango wa kuimarisha kiwanja kidogo cha ndege cha Kigunda, Mkoa wa Kaskazini Unguja ili kubeba ndege kubwa kuliko kilivyokuwa sasa.

 Akizungumza katika uzinduzi huo wa kurejesha huduma katika kiwanja hicho ambazo zilisitishwa kwa muda wa miezi mitatu sasa, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud, alisema kurudi kwa huduma za ndege katika kiwanja hicho ambazo zitaweza kurahisisha wageni kufika hoteli kwa muda mfupi.

Alisema kufunguliwa kwa kiwanja hicho kutafungua fursa kwa wageni na wenyeji kufika kwa urahisi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na kuendelea ndani ya Tanzania kwa urahisi.

Aidha alisema kurudisha huduma hizo, zitaweza kuinua uchumi wa nchi pamoja na matumizi mazuri wa muda pamoja na utumiaji huduma za safari kwa wageni.

“Hapa leo tupo Kigunda Mgeni au mwananchi atakapoondoka kwa ndege kutoka hapa hadi Dar-es Salam anahitaji kutumia wastani wa dakika 20 kwa kutegemeana kwa ukubwa wa ndege ambapo utarahisisha kupunguza masafa ya ndege” alisema.

Aidha alisema kurudishwa kwa huduma hizo unafungua fursa za safari kwa wageni na wenyeji wanaotoka Mkoa wa Kaskazini Unguja kuelekea mahali kwengine ndani ya Tanzania.

Hivyo, aliwaomba mashirika ya ndege kuendelea kihimizana wanapopata kiwanja cha Kigunda kipo wazi na kipo tayari kwa ajili ya kupewa huduma ambapo wageni wao walikuwa wakisubiri kwa hamu kiwanja hicho kirejee kutoa huduma.

Aidha alisema kuwa ipo haja kwa kiwanja hicho kutanuliwa na kuwataka wawekezaji waone umuhimu wa kuwekeza katika kiwanja hicho kwani hawatojutia.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Rahma Kassim Ali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Amour Hamil Bakari, alisema kuwa wizara itajitahidi kuzidi kuimarisha uwanja huo ili kuweza kurahisisha huduma za usafiri katika Mkoa huo ikizingatiwa kuwa watalii wengi wanafikia maeneo hayo.

Aidha alisema kuwadhamira ya kuwepo uwanja huo ni kurahisisha huduma za usafari hasa wageni watalii ambao wanakuja upande wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo kumekuwa na hoteli nyingi katika mkoa huo.

Hivyo, alisema kwa sasa wameanza na sasa wizara imejipanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya viwanja vya ndege kuweza kuimarisha zaidi uwanja huo kwa kuweza kubeba ndege kubwa zaidi ya ndege zinazofika katika kiwanja hicho.

Alisema kuwa mipango ya baadae ndege kubwa ziweze kutua katika kiwanja hicho.

Hivyo, alisema kuwa wizara inahitaji mashirikiano ya serikali ya mkoa na wilaya ya kaskazini ‘A’ katika kuhakikisha kwamba dhamira ya serikali inafikiwa ambayo inalenga zaidi katika kuinua uchumi wa nchi ambapo matarajio yao wageni wengi wataingia kwa kutumia usafiri wa ndege na kupelekea kupunguza msongamano wa magari wanayopeleka watalii ukanda wa Kaskazini Unguja.

Nae, Rubani wa ndege iliyofika kwa ajili ya kuchukua abiria katika kiwanja hicho, kutoka kampuni ya ndege ya Safari Plus aina ya B1900D, alisema ni mara ya kwanza kufika katika kiwanja hicho lakini unaonekanwa vizuri na waliweza kuukagua uwanja kabla ya kutua na kuona upo sawa kwa ajili ya kutua bila ya shida.

Hata hivyo, alisema kuwa uwanja huo unakidhi kwa mahitaji ya huduma za awali na imani yao kuwa baadae ukiboreshwa utakuwa imara zaidi.

 

 

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.