WADAU WA TEHAMA ZANZIBAR WAKUTANA.
12 Apr 2021

WADAU WA TEHAMA ZANZIBAR WAKUTANA.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

                                                                                                                                                                                                                                                                             Naibu katibu Mkuu Mifumo ya Kodi na Fedha Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Rashid Said Rashid akifungua na kufunga mkutano wa wadau wa TEHAMA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mkurugenzi Idara ya Mawasiliano Dr Mzee Suleiman Mndewa akitoa maelezo kwa wadau wa TEHAMA huko ukumbi wa shekh Idris Abdul Wakil Kikwajuni mjini Zanzibar

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Wadau wa TEHAMA kutoka taasisi mbali mbali wakiskiliza kwa umakini maelezo yanayotolewa ukumbini hapo

Serikali ya mapinduzi Zanzibar inatarajia kuanza kutumia mifumo ya TEHAMA katika huduma mbali mbali kuanzia mwezi June mwaka huu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na utunzaji wa kumbukumbu na kuondokana na risiti za mkononi. Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Mifumo na Kodi na Fedha Afisi ya Rais fedha na Mipango Zanzibar Rashid Said Rashid katika mkutano na wadau wa TEHAMA na kuwahimiza maafisa TEHAMA wa Serikali kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mabadiliko ya kidigitali ni mkutano uliowakutanisha wadau wa TEHAMA wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa kisiwa Cha Unguja ambapo Naibu Katibu Mkuu mifumo ya kodi na fedha akatumia mkutano huo kuwataka maafisa Tehama kutambua kwamba kwa sasa serikali inataka kuendeshwa kimtandao hivyo wanawajibu wa kubadilika katika  kazi zao.

Mkutano kama huo unatakiwa kufanyika kisiwa Cha Pemba mwezi ujao ukiwa na lengo la kuwafahamisha maafisa Tehama wa Serikali kujua wajibu wao juu ya mfumo wa kidigitali wa Serikali.

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.