Ziara ya mh. Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Terminal II
21 Apr 2021

Ziara ya mh. Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Terminal II

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mh Rahma Kassim Ali akikagua maduka ya biashara  yaliyomo ndani ya uwanja wa Abeid Amani Karume Terminal II

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe Rahma Kassim Ali amesema ataunda kamati maalum ya kuhakiki upya mita za mraba kwenye maduka ya biashara yalipo ndani na nje ya jengo la abiria la  Terminal ll  la uwanja wa Abeid Aman Karume international Airport Zanzibar .
Waziri Rahma amesema hayo leo alipofanya ziara ya kutembelea maduka hayo ambapo alisema kuna haja ya kufanyiwa uhakiki ili aweze kujiridhisha kama utaratibu umefuata   kwa wafanyabiashara wote wanaofanya shuguli za biashara kiwanjani hapo.
Aidha alisema hatua hiyo imefuatiwa baada ya kubaini kuwa huenda kuna ubadhirifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya watendaji wa Mamlaka jambo ambalo amesema hatoweza kulifumbia macho.
Katika hatua nyengine Mhe Rahma amemuagiza Naibu Mkurugenzi wa mamlaka wa viwanja vya ndege Zanzibar Fadhil Juma Ali kuwaondosha katika sehemu zao za kazi Afisa sheria ndugu Lila Ramadhan Silima na Afisa  Biashara ndugu Ridhwan Mohamed Iddi kwa kile kinacho onekana kuzembea katika kutekeleza majukumu yao na kumtaka Mkurugenzi huyo kutafuta watu wengine wazibe nafasi zao na wao kupangiwa kazi nyengine.
 Aidha alisema baada ya kupokea ripoti ya  mikataba kutoka kwa kamati maalum iliyoundwa kipindi cha nyuma ndipo alipoona kuna haja sasa ya kupitia kwa kina mikataba yote ya kibiashara inayofanywa kiwanjani hapo  ndani na nje ya jengo hilo  kwa  lengo la kujidhizisha mwenyewe.
Sambamba na hayo Mhe Waziri alisema atawaandikia barua Kitengo cha kuzuia Rushwa ZAECA kwa vile amebaini kuna mwanya wa rushwa ili nao wakafanye uchunguzi wao kuhusu kadhia hiyo na mara tu watakapomaliza kazi hiyo na kutoa ripoti yao hatua nyengine za kisheria zitafuata.

 

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.