Naibu katibu mkuu wizara ya habari mawasiliano na teknolojia ya habari wa jamuhuri ya muungano waTanzani ndugu Mohammed Khamis Abdalla amewataka watendaji wa zoezi la ukusanyaji wa taarifa za anuani za makazi, nguzo za mitaa na barabara kuhakikisha kwamba wanakamilisha taratibu zote zilizowekwa ili kukamilika kwa wakati
Naibu katibu mkuu wizara ya habari mawasiliano na teknolojia ya habari wa jamuhuri ya muungano waTanzani ndugu Mohammed Khamis Abdalla amewataka watendaji wa zoezi la ukusanyaji wa taarifa za anuani za makazi, nguzo za mitaa na barabara kuhakikisha kwamba wanakamilisha taratibu zote zilizowekwa ili kukamilika kwa wakati.
Naibu waziri wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchkuzi Mhe. Juma Makungu Juma akiwa na viongozi wengine juu ya mnara (Mnara wa Kigomasha) unatumika kwa ajili ya kuongozea meli akiwa ziarani Kisiwani Pemba.
Zoezi la uwekaji wa lami katika barabara ya maeneo huru ya uwekezaji Micheweni tayari limeanza na linaendelea vizuri.
Mchakato wa uwekeaji wa lami nyepesi katika barabara ya Kipapo-Mgelema umekamilika ambapo kwa sasa wajenzi wa barabara hiyo (Wakala wa barabara Zanzibar) wanaendelea na ujenzi wa madaraja kwa ajili ya kuikamilisha ujenzi huo.
Ujenzi wa Barabara ya Chakechake- Wete yenye urefu wa kilomita 22.1 ambapo mchakato wa kuondosha nyumba na vizuwizi unaendelea.
Mchakato wa uondoshaji wa miti kwa ajili ya ujenzi wa barabara katika barabara ya Chakechake- Wete unaendelea.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed ametoa wito kwa wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano katika kukamilika kwa miradi inayotekelezwa na Serikali, wakati akiwa katika ziara maalum ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara pamoja minara ya mawasiliano inayojengwa katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Nd. Amour Hamil Bakari (kulia) akisaini Mkataba wa maridhiano ya Viwanja vya Ndege na Kampuni ya DNATA kutoka Dubai