Mhe. Rahma Kassim Ali
Waziri Wa Wizara Ya Ujenzi, Mawasiliano Na Uchukuzi
Hafla ya utiaji saini baina ya Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupiti Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Kampuni ya Simu ya Zantel iliyoshuhudiwa na Mawaziri na Makatibu Wakuu wa pande zote mbili (SMT na SMZ) iliyokua na dhumuni la Ujenzi wa Minara ya Simu kwa maeneo ambayo hayana Mawasiliano ya simu Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Rahma Kassim Ali amesema kukamilika kwa Uwanja Mpya wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kutoka kwa mkandarasi BCEG China itakuza uchumi wa Zanzibar.
Picha ya pamoja Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na Wakandarasi wa Jengo Jipya la 3 la Viwanja vya Ndege
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Nd. Amour Hamil Bakari alikabidhi rasmi Mkataba wa Jengo jipya la "Terminal " 3 kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nd. Seif Abdalla Juma.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Nd. Amour Hamil Bakari (kulia) akisaini Mkataba wa maridhiano ya Viwanja vya Ndege na Kampuni ya DNATA kutoka Dubai
Wizara ya Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi wametiliana saini Mkataba wa Mashirikiano wa Uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume baina ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege - Zanzibar na Kampuni ya DNATA ya Dubai iliyofanyika Ikulu - Zanzibar.


Amour Hamil Bakari
Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Ujenzi, Mawasiliano Na Uchukuzi
Historia

Utangulizi

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ni miongoni mwa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Wizara hii imeundwa na Idara nne, pamoja na Taasisi Saba zinazojitegemea, Idara hizo ni: - Idara ya Utumishi na Uendeshaji, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Idara ya Mawasiliano na Ofisi Kuu Pemba. Taasisi zinazojitegemea ni Shirika la Bandari, Shirika la Meli, Mamlaka ya Usafiri Baharini, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Wakala wa Mkonga wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Wakala wa Barabara, na Wakala wa Karakana Kuu ya Magari.

MAJUKUMU YA WIZARA
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji imepewa jukumu la kusimamia Sekta ya Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar. Sekta ya Usafirishaji inajumuisha usafiri wa Nchi kavu, Anga na Baharini. Sekta ya Mawasiliano inajumuisha usimamizi wa miundombinu na huduma za Mawasiliano Zanzibar. Wizara inaendelea kusimamia utekelezaji wa majukumu yake kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo (Vision 2020), MKUZA III, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 – 2015 pamoja na mwaka 2015 – 2020, Sera ya Taifa ya Usafiri Zanzibar (2008), Sera ya TEHAMA (2013) na Mpango Mkuu wa Usafiri (Zanzibar Transport Master Plan) 2009.

DIRA

Kuwa taasisi ya umma yenye kuongoza katika kujenga uchumi imara wa Zanzibar kwa kuimarisha miundombinu na huduma za usafiri na mawasiliano

Kukuza na kusimamia miundombinu na huduma za usafiri na mawasiliano zenye kukidhi mahitaji ya wadau wote kulingana na viwango vya Kitaifa na Kimataifa

MAADILI MAKUU
Utiifu. Uwajibikaji. Kujitolea. Uvumbuzi. Uzalendo. Mashirikiano. Uadilifu. Uwazi. Kuzingatia Taaluma.

MALENGO YA WIZARA

  1. Kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma bora na endelevu za Usafiri na Mawasiliano

  2. Kuhakikisha uwepo wa usalama katika mfumo wa Usafiri wa Barabara, Anga na Baharini.

  3. Kuimarisha uwezo wa Taasisi katika kutoa huduma kwa ufanisi.

  4. Kuhakikisha upatikanaji wa Miundombinu ya Usafiri na Mawasiliano iliyobora salama na yenye kufanyakazi.

  5. Kutoa elimu kuhusiana na masuala ya mtambuka ikiwemo maambukizo ya maradhi hatari hususan Ukimwi kwa watumishi na wadau wengine wa Sekta ya Usafiri na Mawasiliao.

  6. Kukuza matumizi ya Teknologia ya Habari na Mawasiliano kwa Taasisi zote pamoja na jamii kwa ujumla.

  7. Kuhusisha masuala ya jinsia katika kuimarisha huduma za usafiri na Mawasiliano.