Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohame akipata maelezo kutoka Mjenzi wa Kampuni ya IRIS kutoka Nchini Uturuki wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Fuoni-Mwera kituo cha Polisi.
Waziri Dk. Khalid akizungumza na Viongozi wa Shirika la Posta la Oman waliofika Afisini kwake Kisauni kwa ajili kusamiliana nae ambapo Mhe. Waziri aliwaeleza Viongozi hao juu ya umuhimu wa mashirikiano ya pamoja katika masuala ya kibiashara kupitia mashirika ya Posta baina ya Tanzania na Oman.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Posta la Oman pamoja na viongozi wengine wa Shirika la Posta Tanzania na baadhi ya viongozi wa Wizara wakati walipofika katika Afisi za Wizara hiyo Kisauni Zanzibar.
Waziri Dk. Khalid akizungumza na waandishi wa habari mara baada kufungua rasmi kikao cha kuandaa muundo wa mfumo wa kieletroniki utakaotumika katikaShirika la bandari Zanzibar.
Mchakato wa uwekeaji wa lami nyepesi katika barabara ya Kipapo-Mgelema umekamilika ambapo kwa sasa wajenzi wa barabara hiyo (Wakala wa barabara Zanzibar) wanaendelea na ujenzi wa madaraja kwa ajili ya kuikamilisha ujenzi huo.
Ujenzi wa Barabara ya Chakechake- Wete yenye urefu wa kilomita 22.1 ambapo mchakato wa kuondosha nyumba na vizuwizi unaendelea.
Mchakato wa uondoshaji wa miti kwa ajili ya ujenzi wa barabara katika barabara ya Chakechake- Wete unaendelea.