OFISI KUU PEMBA.
Ofisi kuu Pemba ni moja kati ya Idara zinazounda Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zaanzibar.
Idara hii inaongozwa na Ofisa Mdhamini, ambae kwa sasa ni Hamad Ahmed Mohamed Baucha.
Lego kuu la Ofisi kuu Pemba:
Kuhakikisha kuwa majukumu ya Wizara yanatekelezwa kwa upande wa Pemba.
Kazi kubwa ya Ofisi Kuu Pemba ni kuratibu kazi za Wizara ambapo hufanya kazi zifuatazo.
- Kuratibu Ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara.
- Kuratibu na kusimamia huduma za Usafiri Barabarani .
- Uratibu wa Huduma za Teknolojia ya habari na Mawasiliano (TEHAMA).
- Uratibu na usimamizi wa Mipango na bajeti.
- Uratibu wa Maslahi na Maendeleo ya Rasilimali watu.
- Uratibu wa Mashirika na Taasisi zinazojitegemea za Wizara
Ofisi Kuu Pemba inaratibu kazi za Idara nyingine zote za Wizara kwa Pemba. Idara hizo zinasimamiwa na Waratibu ambao humsaidia Ofisa Mdhamini katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Waratibu hao ni:-
- Mratibu wa Idara ya Mipango Sera na utafiti.
- Mratibu wa Idara ya Utumishi na uendeshaji.
- Mratibu wa Idara ya Usafiri na Leseni.
- Mratibu wa Idara ya Ujenzi na utunzaji wa Barabara,ambae pia ni Muhandisi Mkaazi.
- Mratibu wa Idara ya Mawasiliano.
Kwa sasa Ofisi Kuu Pemba inaratibu Utekelezaji wa Miradi Miwili ya Maendeleo ambayo ni
- Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Ole –Kengeja (Km 35).Barabara hii inajengwa kwa kiwango cha lami,na inajengwa na Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara( UUB), na Inasimamiwa na Mshauri Mwelekezi (Consultant) Kampuni ya CAPSEL ya Daresalam.
- Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Chake –Wete (Km 22) ambayo inatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.Hatua za matatayarisho ya Ujenzi wa barabara hii zinaendelea.
Aidha Ofisi Kuu inaendelea kuratibu kazi za matengenezo ya barabara mbalimbali Kisiwani Pemba.