DK.SHEIN AMEFUNGUA BARABARA YA KIWANGO CHA LAMI KUTOKA BUBUBU HADI MKOKOTONI.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria kuifungua barabara ya Bububu hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, iliojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya (CCECC ) kutoka Nchini China
DK.SHEIN AMEFUNGUA BARABARA YA KIWANGO CHA LAMI KUTOKA BUBUBU HADI MKOKOTONI.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikata uteke kuashiria kuifungua barabara ya Bububu hadi Mkokotoni iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya Ujenzi kutoka Chini ya (CCECC) (kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Mhe.Dkt, Sira Ubwa na Mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi (CCECC) Kanda ya Afrika Mashariki Bw.Zhang Junle na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu Ndg. Mustafa Aboud Jumbe na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Meneja Mkaazi Bw.Alex,M.Mubiru
Rais wa Zanzibar Dk.Shein afungua Daraja la Kibondemzungu barabara ya Fuoni Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Daraja la Kibonde Mzungu Wilaya ya Magharibi "B" Unguja (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Mhe Dkt. Sira Ubwa na (kulia kwa Rais Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi,Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar.Dr. Abdalla Juma Mabodi na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Ndg. Mustafa Aboud Jumbe.
Rais wa Zanzibar Dk.Shein afungua Daraja la Kibondemzungu barabara ya Fuoni Zanzibar
uzinduzi wa Daraja la Kibondemzungu barabara ya Fuoni Zanzibar
uzinduzi wa Daraja la Kibondemzungu barabara ya Fuoni Zanzibar
UZINDUZI WA MT. UKOMBOZI II.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Damen Shipyard Gorinchem, Kanda ya Afrika Mr.Ronald Maat, alipowasili katika viwanja vya Bandari ya Malindi Zanzibar kwa ajili ya Uzinduzi wa Meli ya Mafuta ya MT.Ukombozi II, hafla hiyo imefanyika
UZINDUZI WA MT. UKOMBOZI II.
Rais wa Zanzibzr na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr ALI MOHAMED SHEIN akikata utepe kuashiria kuizindua rasmi Meli mpya ya mafuta MT UKOMBOZI 2 akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji kushoto Dr Sira Ubwa Mamboya
UZINDUZI WA MT. UKOMBOZI II.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kulia kwa Rais Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe na kushoto kwa Rais Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dr. Sira Ubwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, wakimsikiliza Msaidizi Nahodha wa Meli ya MT.Ukombozi II Ndg. Ameir Zuberi Kombo,akitowa maelezo wakati wa kutembelea moja meli hiyo baada ya uzinduzi wake uliofanyika leo katika bandari ya Malindi Zanzibar.
UZINDUZI WA MT. UKOMBOZI II.
KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Ndg. Mustafa Aboud Jumbe, akitowa maelezo ya kitaalamu ya Uundaji wa Meli ya Mafuta ya MT. Ukombozi II, wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Meli hiyo uliofanyika katika bandari ya Malindi Zanzibar.
UZINDUZI WA MT. UKOMBOZI II.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya sherehe za Uzinduzi wa Meli Mpya ya Kisasa ya Mafuta ya MT. Ukombozi II, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika bandari ya Malindi
KIKAO CHA KAMATI YA ARDHI NA MAWASILIANO YA BARAZA LA WAWAKILISHI
Kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango- Gombani Kisiwani Pemba
WAZIRI WA UJENZI USAFIRISHAJI NA MAWASILIANO ZANZIBAR DR SIRA UBWA MAMBOYA AVUNJA BODI YA SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bandari Zanzibar
ZIARA YA WAZIRI WA UJENZI USAFIRISHAJI NA MAWASILIANO ZANZIBAR DR SIRA UBWA MAMBOYA KATIKA BARABARA YA OLE-KENGEJA
ZIARA DODOMA
.Mhe Waziri akipokea maelekezo kuhusu mnara wa mawasiliano wa makanda kutoka kwa ndugu Kaimu mtendaji Mkuu wa Mfuko wa mawasiliano kwa wote ndugu Jostina Mashiba
UTIAJI SAINI WA MELI MPYA YA MAFUTA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa SMZ Nd Khamis Mussa akisaini makabidhiano ya kiufundi ya Meli mpya ya kubeba mafuta "Ukombozi II" leo jijini Shanghai.
MELI MPYA YA MAFUTA
Meli mpya ya kubeba mafuta "Ukombozi II"
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN, AFUNGUA BARABARA KIYUNI HADI NGOMENI PEMBA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Barabara mpya ya kiwango cha lami kutoka Kiyuni hadi Ngomeni Wilaya ya Chake Chake Pemba kulia Mke wa Rais wa Rais Mama Mwanamwema Shein, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe na kushoto Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe. Dr, Sira Ubwa Mwaboya.
UZINDUZI WA BARABARA YA MKANYAGENI KANGANI WILAYA YA MKOANI PEMBA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa Kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Barabara ya Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba leo.kushoto Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Mhe. Sira Ubwa Mwamboya.
UZINDUZI WA BARABARA YA MKANYAGENI KANGANI WILAYA YA MKOANI PEMBA
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Zanzibar Ndg. Mustafa Aboud Jumbe, akisoma taarifa ya kiufundi ya ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami kutoka Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba, baada ya kufunguliwa barabara hiyo leo.
SERIKALI YAPOKEA VIFAA VYA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO
Muonekano halisi wa Mtambo wa kuchanganyia Lami uliotoka Nchini Brazil unavyoonekana
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS KATIBA SHERIA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA AWEKA JIWELA MSINGI DARAJA LA KIBONDEMZUNGU ZANZIBAR
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe akitoa maelezo ya Kitaalam kuhusiana na Ujenzi wa Daraja la Kibondemzungu Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

IDARA YA USAFIRI NA LESENI.

1.0 Utangulizi

Baada ya Mapinduzi matukufu ya Januari 1964 huduma za usafiri na mawasilino zilikuwa chini ya iliyokuwa Wizara ya Kazi, Ufundi, Njia na Simu. Kwa nyakati tofauti shughuli za sekta ya usafiri na mawasiliano zilikuwa zikijumuishwa pamoja na sekta nyengine kama vile ujenzi, ufundi na nyenginezo..

Mwaka 1978 ilibadilishwa jina na kuitwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ambayo ilidumu hadi mwaka 2010 ilipobadilishwa jina na kuitwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na mwaka 2016 ikabadilishwa tena jina na kuitwa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji.

Idara ya Usafiri na Leseni ilianzishwa mwezi Juni mwaka 2001 chini ya iliokuwa Wizara ya Mawasilisno na Uchukuzi ikifanya kazi kwa kutumia sheria iliorithiwa kutoka kwa wakoloni ijulikanayo kama ‘Road Traffic Decree cap 35’. Idara ilianzishwa kwa lengo la kusimamia shughuli zote za usafiri wa barabarani katika visiwa vya Unguja na Pemba, Kusimamia Bohari kuu za serikali Unguja na Pemba pamoja na kuendesha Karakana Kuu na sehemu za mitambo ziliopo Malindi Unguja na Cahake chake Pemba.

Mwaka ( 2003) Sheria nambari 7 ya Usafiri barabarani ilipitishwa rasmi ilioipa mamlaka Idara ya Usafiri na Leseni kutekeleza majukumu yake yanayohusiana na usafiri wa barabarani katika visiwa vya Zanzibar.

1.1 SEHEMU ZA IDARA

Idara ya Usafiri na Leseni imegawika katika sehemu zifuatazo:-

 • Ofisi kuu ya Idara iliyopo Mwanakwerekwe.
 • Sehemu ya Karakana kuu iliyopo Chumbuni.
 • Sehemu ya Upasishaji wa vyombo vya moto iliopo Karakana.
 • Sehemu ya Idara iliyoko Chakechake Pemba.

1.2     MAJUKUMU YA IDARA

Majukumu makubwa ya Idara hii ni haya yafuatayo:-

 • Kusimamia Sekta ya Usafiri barabarani.
 • Kukagua na kupasisha vyombo vya moto vinavyotumia barabara.
 • Kuwafanyia majaribio ya nadharia na vitendo madereva wanafunzi.
 • Kutoa leseni kwa madereva wanafunzi, vyuo vya udereva, walimu wa skuli za udereva
 • Kutoa leseni kwa magari ya biashara.
 • Kutoa ruhusa za njia na usafirishaji.
 • Kutoa beji za Utingo na Madereva
 • Kutoa vibali kwa magari na wageni wanaoendesha Zanzibar.
 • Kuendesha na kusimamia karakana kuu ya Serikali iliyoko Chumbuni na sehemu ya mitambo iliyoko Pemba.
 • Kusimamia shuhuli za Bodi ya Usafiri Barabarani na Kamati ya Kitaifa ya wiki ya Usalama Barabarani.

1.2.1. UTOAJI WA LESENI ZA KUENDESHA VYOMBO.

Muombaji wa leseni ya kujifundishia chombo cha moto anatakiwa kupitia hatua tatu ili kupata leseni ya kuendesha chombo.

(i) Kukata leseni ya kujifundishia(leaner’s license, ili kupata leseni ya kujifundishia muombaji anatakiwa kuwasilisha maombi ya kupatiwa leseni ya kujifundishia (Learner’s Lisence)baada ya kufanya mambo yafuatayo:-

 • Kujiunga na Chuo cha Udereva ili kupata mafunzo ya kuendesha chombo.
 • Kufanya uchunguzi wa afya yake katika Hospitali za Serikali. Kuwasilisha picha mbili ‘‘passport size’’ ambazo hajavaa kofia kwa mwanamme na awe hajavaa nikab (hajafunika uso) kwa mwanamke.
 • Kopi ya kitambulisho cha Mzanzibari/Passpoti au Cheti cha kuzaliwa.

(ii) MITIHANI YA NADHARIA.

Hatua ya pili kwa muombaji wa leseni baada ya kupata leseni ya kujifundishia (Learner’s lisence) ni kufanya mitihani ya nadharia ambayo imegawika sehemu mbili:

(i) Alama za barabarani (Road signs and symbols).

(ii) Sheria za barabarani.

Kila mtahiniwa analazimika kulipia na kufanya mitihani na kupata alama sabiini(70%) kila sehemu ili kuendelea na hatua ya kufanya mitihani ya vitendo (Practical driving test).

Iwapo mtahiniwa hakupata alama 70% sehemu moja au zote mbili atalazimika kuerejea mtihani aliokosa alama 70.

 (iii) MITIHANI YA VITENDO.

Mtihani wa vitendo ni hatua ambayo muombaji wa leseni hujaribiwa kwa vitendo uelewa wake wa sheria na alama za barabarani, mtahiniwa huyo hutakiwa kulipia mtihani wa vitendo, na kufanyiwa mambo yafuatayo:-

 • Kujaribiwa uwezo wake wa kuona kabla ya kuanza majaribio ya kuendesha chombo (visual test).
 • Kufanyiwa mtihani wa awali (Pre test) kuangalia iwapo gari anayotaka kufanyiwa majaribio inafaa kwa shughuli hiyo.
 • Kufanyiwa mtihani wa kuendesha ndani (indoor test)
 • Kufanyiwa mtihani wa nje (out door test)

Iwapo Mkaguzi amethibitisha kuwa mtahiniwa anaelewa vyema sheria na alama za barabarani kwa kupata alama 70 au zaidi humpatia cheti cha matokeo (statement of results) kinachotumika kutayarishia cheti cha umahiri (Certificate of competence) ambacho kitatumika kutengenezea leseni kulingana na daraja aliloomba.  

1.2.2. UKAGUZI WA VYOMBO VYA MOTO.

Idara ya Usafiri na Leseni inafanya ukaguzi wa vyombo va moto vinavyotumia barabara ili kuangalia uzima wa vyombo, ukaguzi huo uko wa aina nne.

 1. Ukaguzi wa mwaka (Annual inspection)
 2. Ukaguzi wa ajali
 3. Ukaguzi wa shaka.
 4. Ukaguzi maalum

Ukaguzi wa mwaka: Ukaguzi huu hufanyika kwa kila chombo cha moto kinaoptaka kuingia barabarani na kinapofikia mwaka tokea kilipopasishwa awali, ukaguzi huu unafanyika ili kuweza kuangalia uzima wa chombo kutokana kutumika kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Ukaguzi wa ajali: Ukaguzi huu hufanyika kila inapotokea ajali ili kubaini uzima wa chombo na chanzo cha ajali iliyotokana na chombo husika pamoja na kuangalia leseni ya dereva.

Ukaguzi wa shaka: Ukaguzi huu hufanyika muda wowote ikitokea chombo cha moto kuhusiana na kimetiliwa mashaka uzima wake, chombo hicho huchukuliwa na kupelekwa kwa mkaguzi ili kikaguliwe iwapo kinafaa kutembea barabarani au hakifai.

Ukaguzi wa maalum: Ukaguzi huu hufanyika muda wowote inapoonekana kuna umuhimu wa kufanya hivyo ili kuangalia mambo mbali mbali yanayohusu taratibu za usafiri wa barabarani, kama kuangalia hati mbali mbali za kufanyia biashara ya kusafirisha abiria na mizigo pamoja na uzima wa vyombo.

1.2.3. LESENI ZA MAGARI YA BIASHARA    

Idara ya Usafiri na Leseni inatoa leseni za magari ya biashara ya aina nane kama zifuatazo:-

 1. Daladala (Town bus)
 2. Shamba (Stage bus)
 3. Private hire
 4. Magari ya wafanyakazi
 5. Magari ya wanafunzi
 6. Taxi
 7. Magari ya kukodisha na kuendesha mwenyewe (Hire and Drive)
 8. Mizigo A na Mizigo C ( Mizigo A gari za biashara na Mizigo C ya nyumbani).

Muombaji wa leseni ya gari ya biashara anatakiwa kufanya mambo yafuatayo ili kupatiwa leseni hiyo:-

Gari liwe limepasishwa.

Gari liwe limekatiwa bima.

Gari liwe linajuilikana katika halmashauri husika (kwa daladala na shamba).

Gari likatiwe leseni ya njia (road lisence)

1.2.4.UTOAJI WA VIBALI KWA MADEREVA WENYE LESENI ZA KIGENI

Wageni wanaohitaji kuendesha vyombo vya moto Zanzibar ambao nchi zao zimeridhia mkataba wa Geneva wa mwaka 1949 na Viena wa mwaka 1968 leseni zao zinatambuliwa na hupewa vibali vya utambulisho kuendesha vyombo Zanzibar.

Mhusika kutakiwa kuwasilisha leseni yake ili kuthibitishwa (verification) kabla ya kupewa kibali.

1.2.5.BEJI ZA UTINGO NA MADEREVA

Idara ya Usafiri na Leseni inasimamia watoaji wa huduma za usafirishaji wa abiria kwa kuwapatia beji Utingo na Madereva. Dereva hutakiwa kujaza mkataba maalum wa utoaji wa huduma hiyo, kuwasilisha kopi ya leseni yake, kitambulisho cha Mzanzibari pamoja na picha mbili ‘pasport’ size.

Utingo hutakiwa kujaza mkataba kuwasilisha kitambulisho cha Mzanzibari pamoja na picha mbili ‘’passport size’’.

 1.2.5. SEHEMU YA KARAKANA

Karakana Kuu ya Serikali na sehemu ya Mitambo ilioko Pemba zinahusika na utengenezaji wa vyombo vya moto vya watu binafsi na Serikali.

Kazi zinazotekelezwa Karakana Kuu ni kama zifuatazo:-

 1. ‘‘Injection section’’, sehemu hii inahusika na kurekebisha, kubadilisha na

         kuzifanyia marekebisho injector pumps pamoja na nozzle.

 1. ‘‘Service section’’, hii ni sehemu inayohusika na kuzifanyia matengenezo ya utunzaji, umwagaji wa oil, maji ya betri, engine oil, diesel na petrol filer, gear oil na kadhalika ili kuondoa vifaa ambavyo vinaweza kuharibika mwenendo wa chombo.
 1. ‘‘Engine maintenance and repair’’, sehemu hii inahusika na kutengeneza mashine zenye matatizo ya aina mbalimbali

      4. Unyooshaji na utiaji wa rangi, hii ni sehemu ambayo gari lililoathiriwa kama kupata ajali hunyooshwa na kutiwa rangi ili kurejea hali ya kupendeza.

Mawasiliano

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
P.O.Box 266
ZANZIBAR
TANZANIA

AU

190 FUMBA ROAD
POSTCODE: 71201
ZANZIBAR, TANZANIA

email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.