IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI
Idara ya Uendeshaji na Utumishi inaongozwa na Mkurugenzi endeshaji na Utumishi Ndugu Bimkubwa Abdi Nassib.
MAJUKUMU YA MKURUGENZI UENDESHAJI /UTUMISHI
- Kutoa huduma za Uongozi wa Rasilimaliwatu na Utawala kwa Wizara husika
- Kusimamia majukumu ya vitengo vilivyo chini ya Idara
- Kusimamia masuala ya ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo kwa Wafanyakazi wa Wizara
- Kuhakikisha kuwepo kwa watendaji wa kutosha na wenyesifa na kuweka kumbukumbu za masuala mbalimbali yanayohusu watendaji
- Kufanya tathmini ya utendaji wa kila Mtumish iwa Wizara na kuandaa ripoti ya hali ya Utumishi kila baada ya muda kwa mujibu wa sheria au maagizo maalum
- Kuratib masuala Mtambuka yakiwemo Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya hali ya nchin.k
- Kutoa huduma za kitaaluma na huduma za manunuzi na uhifadhi wa vifaa kwaajili ya Idara nyengine
- Kutoa huduma za uhasibu ikiwa ni pamoja na uwekaji wa kumbukumbu za hesabu, mapato na manunuzi, ulipaji wa mishahara, na matayarisho ya mafao ya uzeeni
- Kuandaa na kusimamia mpango kazi wa Idara
- Kufanya kazi nyengine kama zitakavyoelekezwa na uongozi wa Wizara kwa mujibu wa sheria na kanuni za kazi
Idara ya Uendeshaji na Utumishi ina vitengo vitatu kama vifuatavyo:-
- KITENGO CHA UENDESHAJI
MAJUKUMU YAKE
- Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu katika sehemu ya kazi
- Kusaidia kusimamia nidhamu ya Wafanyakazi
- Kuaiisha matatizo ya Wafanyakazi
- Kusimamia matumizi na matunzo ya vifa vya Wizara ikiwemo vyombo vya usafiri, magari, mitambo,samani,vifaa vya kuandikiana vifaa vya mawsiliano
- Kusimamia majego na mali nyengine zisizohamishika
- Kusimamia shughuli za kiufundi na uendeshaji wa maghala ya Wizara
- Kufanya kazi zote atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
2. KITENGO CHA UTUMISHI
MAJUKUMU YAKE
- Kutunza kumbukumbu za watumishi wote kulingana na mahalalipo
- Kukusanya takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya Watumishi
- Kusaidia kukadiria idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo
- Kufanya kazi zote atazopangiwa na mkuu wake wa kazi
- KITENGO CHA UTUNZAJI KUMBUKUMBU
MAJUKUMU YAKE
- Kutafuta kumbukumbu /nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji
- Kudhibiti upokeaji , uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka
- Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na nasomohusika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi
- Kuweka /kupanga kumbukumbu/nyaraka katika renki (file racks /cabinets)katika masjala /vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu
- Kuweka kumbukumbu (barua , nyarakan.k)katika mafaili
- Kushughulikia maombi ya kumbukumbu / nyaraka kutoka taasisi za Serikali
- Kufanya kazi nyengine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
Aidha idara inasimamia utekelezaji wa kazi za Ofisi ya Wizara na kuhakikisha kuwa rasilimali zote muhimu zinapatikana kwa wakati na wafanyakazi kuendelea kufanya kazi katika mazingira mazuri na ya kuridhisha. Kazi kwa ajili ya ununuzi wa mashine ya ofisi (kompyuta), vifaa vya (stationeries), samani za ofisi, huduma ya malipo ya maji, umeme na mawasiliano ya simu ya ofisi (simu na mtandao). Zaidi ya hayo Idara hii hutoa huduma za usimamizi wa ofisi na kuhakikisha magari yanapata huduma na matengenezo mengine pamoja na kuyapatia mafuta .
MUUNDO WA IDARA YA UTUMISHI