Amour Hamil Bakari Katibu Mkuu |
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji ilianzishwa mwezi April 2016 baada ya uchaguzi mkuu na kuchukua nafasi ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya zamani.
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji inaundwa na Idara sita, Ofisi Kuu Pemba, Taasisi huru sita na Bodi moja ya Ushauri. Idara hizo ni pamoja na Idara ya Sera, Mipango, na Utafiti, Utawala na Utumishi, Habari na Mawasiliano, Barabara Uchukuzi na Leseni, ujenzi wa barabara na matengenezo na Idara ya Majenzi. Taasisi huru ni Shirika la Bandari la Zanzibar, Shirika la Nyumba, Mamlaka ya Mji Mkongwe, Shirika la Meli la Zanzibar, Mamlaka ya Usafiri Baharini na Mamlaka ya Ndege ya Zanzibar. Bodi ya ushauri ni Bodi ya Usafiri wa Barabara.