BANDARI YA MANGAPWANI
Mradi wa bandari ya matumizi mbalimbali (multipurpose port) utahusisha maendeleo ya miundombinu ya kushughulikia na kuhifadhi mizigo, ikiwemo mizigo ya makontena, CBM pamoja na gati (jetty), hifadhi ya kimkakati ya mafuta na gesi, na vituo vya usafirishaji na usambazaji (logistic centers).
Upembuzi yakinifu (feasibility study) umekamilika, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (RGoZ) ipo katika hatua za mwisho za kuingia mkataba na mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya makontena na mizigo mchanganyiko.