Z
BIG Z Project Fungua Ukurasa
Mwanzo / Kuhusu Sisi
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar

Kuhusu Wizara Yetu

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ni miongoni mwa Wizara muhimu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya miundombinu, ujenzi, usafiri wa nchi kavu, baharini na angani pamoja na huduma zinazohusiana na sekta ya uchukuzi.

Muhtasari

Miundombinu
Barabara, majengo, karakana na huduma za ujenzi.
Uchukuzi
Usafiri wa nchi kavu, baharini na angani.
Taasisi
Idara, vitengo na taasisi zinazotekeleza majukumu ya Wizara.
Utangulizi

Karibu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ina jukumu la kusimamia, kuratibu na kuendeleza sekta za ujenzi na uchukuzi Zanzibar. Wizara inahakikisha uwepo wa miundombinu bora, salama, endelevu na yenye kuchochea ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na maendeleo ya Zanzibar.

Majukumu ya Wizara

Wizara ina dhamana ya kupanga sera, kusimamia utekelezaji wa mipango na kuratibu taasisi zilizo chini yake katika maeneo ya ujenzi, barabara, usafiri wa baharini, usafiri wa anga, usafiri wa barabarani, huduma za bandari, meli, viwanja vya ndege, karakana na miundombinu mingine muhimu ya uchukuzi.

Dira na Mwelekeo

Kuwa taasisi ya umma yenye kuongoza katika kujenga uchumi imara wa Zanzibar kupitia miundombinu ya ujenzi na uchukuzi iliyo bora, salama, jumuishi na inayokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

Dhamira

Kukuza, kuimarisha na kusimamia miundombinu pamoja na huduma za ujenzi na uchukuzi kwa ufanisi, uwazi na ubunifu ili kutoa huduma bora kwa wananchi, taasisi na wadau wote wa maendeleo Zanzibar.

Maadili Makuu

Wizara inaongozwa na maadili ya msingi katika kutoa huduma kwa wananchi na wadau wake.

Utiifu
Uwajibikaji
Uadilifu
Uwazi
Uzalendo
Ubunifu
Mashirikiano
Kujitolea
Kuzingatia Taaluma
Malengo ya Wizara

Malengo ya Kimkakati

Wizara inalenga kuhakikisha huduma na miundombinu ya ujenzi na uchukuzi inachangia moja kwa moja ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

1

Kuhakikisha wananchi na wadau wanapata huduma bora, salama na endelevu za uchukuzi.

2

Kusimamia usalama katika mifumo ya usafiri wa barabarani, baharini na angani.

3

Kuimarisha miundombinu ya barabara, majengo, bandari, viwanja vya ndege na vifaa vya uchukuzi.

4

Kuongeza ufanisi wa taasisi zilizo chini ya Wizara katika kutoa huduma kwa wananchi.

5

Kuhakikisha mipango, sera na tafiti zinatumika katika kuboresha sekta za ujenzi na uchukuzi.

6

Kuzingatia masuala mtambuka kama jinsia, mazingira, usalama kazini na matumizi ya teknolojia.

Muundo wa Taasisi

Muundo wa Wizara

Wizara inaongozwa na Waziri, Katibu Mkuu, Idara, Ofisi Kuu Pemba, Vitengo pamoja na taasisi zinazotekeleza majukumu mbalimbali ya ujenzi na uchukuzi Zanzibar.

MCHORO WA MUUNDO WA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI

Download PDF
WAZIRI
KATIBU MKUU

Idara na Ofisi

  • Idara ya Mipango, Sera na Utafiti
  • Idara ya Uendeshaji na Utumishi
  • Idara ya Mawasiliano
  • Ofisi Kuu Pemba

Vitengo vya Wizara

  • Kitengo cha Uhasibu
  • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
  • Kitengo cha Huduma za Kisheria
  • Kitengo cha Tehama
  • Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano
  • Kitengo cha Ununuzi na Uondoshaji Mali za Umma

Taasisi Zilizo Chini ya Wizara

  • Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
  • Mamlaka ya Usafiri Baharini
  • Mamlaka ya Usafiri Barabarani
  • Shirika la Bandari
  • Wakala wa Barabara
  • Wakala wa Karakana Kuu ya Serikali ya Magari
  • Wakala wa Mkonga wa Mawasiliano
  • Wakala wa Shirika la Meli